Jumapili, 29 Desemba 2013

MH. SUMAYE ACHANGISHA MILIONI 225 UJENZI WA UKUMBI, KANISA KATOLIKI MAWELA


Waumini wa kanisa katoriki Parokia ya Maonano, Mawela wakiwa katika ibada.
Waziri mkuu mstaafu Fredrick Sumaye akitembelea ukumbi wa kisasa unaojngwa katika Parokia hiyo kwa ajili ya shughuli mbalimbali.
Baadhi ya waumini pamoja na wageni mbalimbali waliojitokeza katika harambee ya ujenzi wa ukumbi wa kisasa katika Parokia ya Maonano Mawela.
Mshereheshaji wa shughuli hiyo ya harambee ya ujenzi wa Ukumbi wa kisasa Godwin Gondwe akijaribu kuweka mambo sawa .
Paroko wa parokia ya Maonano ,Mawela Padre Anthony Marunda akisoma risala kwa mgeni rasmi katika harambee ya kuchangia ujenzi wa ukumbi wa kisasa katika kanisa hilo.
Waziri mkuu mstaafu Fredrick Sumaye akizungumza katika harambee ya ujenzi wa ukumbi wa kisasa wa kanisa katoliki Parokia ya Maonano Mawela jana.
Waziri mkuu mstaafu Sumaye pamoja na mshereheshaji wa shughuli hiyo Godwin Gondwe wakijadiliana jambo na mmoja wa wajumbe wa kamati ya harambee ya Ujenzi wa ukumbi huo wa kisasa Anthony Komu.
Waziri mkuu mstaafu Sumaye akimkaribisha Mbunge wa jimbo la Moshi vijijini Dk Cyril Chami kuchangia katika harambee ya Ujenzi wa Ukumbi wa kisasa katika kanisa katoliki Parokia ya Maonano Mawela .

Na Dixon Busagaga wa globu ya jamii Moshi

Waziri Mkuu mstaafu Frederick Sumaye amesema kuwa mwaka 2014 ni mwaka muhimu sana kwa mustakabali wa taifa letu kwa sababu ni mwaka wa uchaguzi katika ngazi za serikali za mitaa na ni mwaka wa maandalizi ya uchaguzi mkuu mwaka 2015, hivyo watanzania wamwombe Mungu awajalie hekima na busara, na kuwapa ujasiri waweze kuchagua viongozi watakaofaa kuongoza kwa hekima, busara, upendo na haki.

Akizungumza na Mamia ya Waumini mbalimbali waliojitokeza katika harambee ya kuchangia ujenzi wa Ukumbi wa Parokia ya Maonano, Mawela katika Jimbo Katoliki la Moshi Sumaye alisema ni ukweli ulio wazi kuwa chaguzi za kitanzania sasa zimegubigwa na rushwa na vishawishi vingi wala siyo ubora, uhodari wala tabia ya anayetaka nafasi ya uongozi.

“Hivi sasa rushwa na matumizi makubwa ya fedha za kuwanunua wapiga kura vinataka kuwa utaratibu halali wa kuwapata viongozi wetu wa ngazi zote kuanzia ngazi za vijiji na mitaa hadi ngazi ya Urais, utaratibu huuu ni wa hatari na lazima tuupige vita kwa pamoja” alisema Sumaye.

Aliongeza kuwa viongozi wanapaswa kuwa wacha Mungu, watu wa kweli, wenye kuchukukia mapato ya udhalimu, hao ndio wanaweza kuwa viongozi kwa kutegemea uwezo wao, upeo wao, uhodari wao, ujasiri wao na uaminifu wao kwa Mungu na kwa jamii wanayoiongoza.

Sumaye alisema pia, Katika utaratibu wa demokrasa sahihi na halisi, wapiga kura hutakiwa kuwachagua viongozi kufutana na sifa nzuri za uongozi alizo nazo, na kuonya kuwa Kiongozi anatafutwa na jamii na siyo yeye kusaka uongozi, mbaya zaidi ni pale msaka uongozi anapotafuta nafasi hiyo kwa njia zisizofaa kama vile rushwa na kununua wapiga kura.

“Uongozi hautafutwi kwa udi na uvumba wala kwa rushwa, leo chaguzi zetu zimegubikwa na rushwa na vishawishi vingi na siyo ubora, uhodari wala tabia ya anayetaka nafasi ya uongozi, rushwa na matumizi makubwa ya fedha kununua wapiga kura vinataka kuwa utaratibu wa kawaida tena halali wa kuwapata viongozi wa ngazi zote kuanzia kijiji hadi Urais, huu ni utaratibu wa hatari na lazima upigwe vita kwa pamoja” aliongeza Sumaye.

Sumaye akinukuu Biblia takatifu (Kut.23:8) inayosema “nawe usipokee rushwa kwani rushwa huwapofusha macho hao wanaonao, na kuyapotoa maneno ya wenye haki” alionya kuwa kama Biblia inasema rushwa inapofusha macho, sisi watanzania tukichagua kiongozi mla rushwa au mtoa rushwa au anayenunua wapiga kura, huyo hawezi kutuongoza tufike tunakotaka, tukichagua kiongozi wa aina hiyo atatumia nafasi yake kujinufaisha yeye na rafiki zake.

Katika hotuba hiyo pia Sumaye alisema watu walioiba wakamatwe na kufungwa maana wametenda jinai, hivyo hivyo waliotoa rushwa au kuifisadi nchi, kuuza madawa ya kulevya au kuua wanatakiwa kutubu kwa kuwa hiyo ni dhambi lakini wakikamatwa waadhibiwe maana hayo yote ni makosa ya jinai,

Katika harambee ya ujenzi wa Ukumbi huo Sumaye alifanikiwa kuchangisha pesa taslimu 55,295,500, na ahadi ya 170,000,000 Jumla ni milioni 225,295,500. Akivuka lengo la harambee hiyo ambayo ilikuwa imepangwa 150,000,000. Gharama halisi za Ukumbi huo wa kisasa wa Parokia ya Mawela ili ukamilike utagharimu 450,000,000/.

WAZIRI MKUU MSTAAFU SUMAYE APINGA RUSHWA KWA NGUVU KWENYE UCHAGUZI.

Rushwa kwenye chaguzi, ufisadi vyamchukiza Sumaye



‘“Ningefarijika sana kama tunaojiandaa kugombea nafasi mbalimbali hasa nafasi ya urais tungekemea rushwa na ufisadi hadharani.” Frederick Sumaye 
Na Daniel Mjema,Mwananchi

Posted  Jumapili,Decemba29  2013  saa 15:34 PM
Kwa ufupi
  • Sumaye alitoa kauli hiyo jana katika harambee ya kuchangia ujenzi wa ukumbi wa Parokia ya Mawela ya Kanisa Katoliki Jimbo la Moshi iliyohudhuriwa pia na Mbunge wa Moshi Vijijini, Dk Cyril Chami.
SHARE THIS STORY

1
Moshi. Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye amesema angefarijika kama wanasiasa wanaojiandaa kugombea Urais mwaka 2015, wangekemea vitendo vya rushwa na ufisadi hadharani.
“Zamani uongozi ulikuwa hautafutwi kwa udi na uvumba wala kwa rushwa, bali anayefaa kuwa kiongozi hutafutwa na jamii husika kutokana na ubora wake na siyo vishawishi vyake,” alisema Sumaye.
Sumaye alitoa kauli hiyo jana katika harambee ya kuchangia ujenzi wa ukumbi wa Parokia ya Mawela ya Kanisa Katoliki Jimbo la Moshi iliyohudhuriwa pia na Mbunge wa Moshi Vijijini, Dk Cyril Chami.
“Ni ukweli uliowazi kuwa, leo chaguzi zetu zimegubikwa na rushwa na vishawishi vingi na siyo ubora, uhodari wala tabia ya anayetaka nafsi hiyo ya uongozi,” alisema Sumaye na kuongeza kusema:
“Hivi sasa rushwa na matumizi makubwa ya fedha za kuwanunua wapiga kura vinataka kuwa utaratibu halali wa kuwapata viongozi wetu kuanzia ngazi za vijiji na mitaa hadi ngazi ya urais.”
Sumaye alisema Tanzania hivi sasa inaingia katika nyakati za uchaguzi hivyo, inahitaji viongozi watakaowaletea Watanzania maendeleo ya kweli na kuondokana na umasikini na udhalimu.
“Lakini kama tutakiuka taratibu sahihi za kuwapata viongozi na badala yake wapiga kura tukanunuliwa kwa kupewa rushwa, basi tujue tutawapata viongozi wala rushwa,” alisema Sumaye.
“Fadhila zimeanza kuwa nyingi, wapiga kura tayari wameanza kupigwa mnada na kupangiwa bei kulingana na uhodari au umuhimu wa nafasi aliyonayo mhusika,” alisisitiza Sumaye.
Sumaye alisema Jamii inapaswa kuyapiga vita mambo hayo kwa nguvu zote na kusema: “Vita hii ni kali na tusipoangalia sauti ya wanaopigana inaweza ikafifishwa na kelele za wanaonufaika na rushwa hizi za nyakati za chaguzi. Inaelekea fedha zinazotumika ni nyingi sana”.
“Ukikemea tu rushwa basi utapachikwa sababu nyingi zisizohusika ikiwemo ya kugombea urais mwaka 2015…nasema katika hili, suala la kugombea au kutogombea urais mwaka 2015 siyo sababu,” alisema.

Alhamisi, 24 Oktoba 2013

RAIS MSTAAFU MHE. BENJAMINI WILLIAM MKAPA AZINDUA KAMPENI YA TUSOME TANZANIA

Friday, October 11, 2013

RAIS MSTAAFU MHE. BENJAMINI WILLIAM MKAPA AZINDUA KAMPENI YA TUSOME TANZANIA (LET US READ TANZANIA CAMPAIGN)

Rais Mstaafu Mhe. Benjamini William Mkapa ambaye pia ni mgeni rasmi akiwasomea hadithi mbalimbali na kuwauliza maswali mbalimbali watoto ambao ni wanafunzi toka shule mmbalimbali leo katika viwanja vya Makao Makuu ya Maktaba ya Mkoa jijini Dar es Salaam.
PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA-MAELEZO.

RAIS Mstaafu Mhe. Benjamini William Mkapa amezindua rasmi Kampeni ya “Tusome Tanzania (Let’s read Tanzania Campaign)iliyoandaliwa na wadau mbalimbali nchini wenye lengo la kuwahamasisha vijana wa kitanzania kujijengea utamaduni wa kusoma vitabu mbalimbali.
Katika uzinduzi huo, Mhe. Mkapa ameipongeza kamati ya wadau waandaaji wa kampeni hiyo kwa kujitoa kwao katika kuhakikisha kuwa watoto wa shule ambao ndiyo taifa la kesho wanapata kujionea wenyewe na anatumaini kuwa watahamasika kupenda kujisomea kwa manufaa ya maisha yao.
“Tabia ya kusoma inamjenga mtu kifikra na kumpa mtu mtazamo”. Alisema Mhe. Mkapa.
Mhe. Mkapa ameongeza kuwa kwa kuwa elimu haina mwisho, kusoma ni namna ya kujielimisha siku hadi siku na kufungua mambo mapya yanayoipa akili changamoto, hivyo amewasisitizia vijana wajijengee utamaduni wa kusoma hasa vitabu vya kiswahili na Kiingereza.
Mmoja wa wadau toka timu ya Let us read Tanzania akimpa maelezo juu ya vitabu mbalimbali viliyotungwa na waandishi mashuhuri ndani na nje ya nchi.
“Someni kazi za Shaabani Robert mwandishi mkongwe wa Tanzania, someni kazi za Mariam Abdallah, Ngugi wa Thio’ngo , Chinua Achebe, Ole Soyinka na .”Alisema Mhe. Mkapa.
Aidha, Mhe. Mkapa ametoarai kwa wadau waandalizi wa kampeni ya “Let’s read Tanzania Campaign” kuwa zoezi hilo lisiishie hapo bali liwe endelevu na kuwafikia watu wengi na haswa vijana, pia amesisitiza kuwa mtandao wa vitabu uhakikishe vitabu hivi vinafika hadi kwenye shule za vijijini na amehamisisha juu ya ujenzi wa Maktaba na kusaidia kuboresha watoto wetu.
Baadhi ya vijana walioshiriki uzinduzi wa Kampeni ya tusome Tanzania (Let us read Tanzania) wakifuatilia kwa makini hotuba toka kwa mgeni rasmi Mhe. Benjamini William Mkapa (hayupo pichani) leo katika viwanja vya Makao Makuu ya Maktaba ya Mkoa jijini Dar es Salaam.

Let’s read Tanzania Campaign ni kampeni iliyoandaliwa na vijana kutoka hasasi mbalimbali lenye lengo la kuwahamasisha vijana wa kitanzania kujijengea utamaduni wa kupenda kusoma vitabu kwa ajili ya kuongeza fikra za vijana na kuwasaidia katika maisha yao.
Source:Na Benedict Liwenga-Maelezo, Dar es Salaam hapo bali liwe endelevu na kuwafikia watu wengi na haswa vijana, pia amesisitiza kuwa mtandao wa vitabu uhakikishe vitabu hivi vinafika hadi kwenye shule za vijijini na amehamisisha juu ya ujenzi wa Maktaba na kusaidia kuboresha watoto wetu.
Baadhi ya vijana walioshiriki uzinduzi wa Kampeni ya tusome Tanzania (Let us read Tanzania) wakifuatilia kwa makini hotuba toka kwa mgeni rasmi Mhe. Benjamini William Mkapa (hayupo pichani) leo katika viwanja vya Makao Makuu ya Maktaba ya Mkoa jijini Dar es Salaam.

Let’s read Tanzania Campaign ni kampeni iliyoandaliwa na vijana kutoka hasasi mbalimbali lenye lengo la kuwahamasisha vijana wa kitanzania kujijengea utamaduni wa kupenda kusoma vitabu kwa ajili ya kuongeza fikra za vijana na kuwasaidia katika maisha yao.
Source:Na Benedict Liwenga-Maelezo, Dar es Salaam hapo bali liwe endelevu na kuwafikia watu wengi na haswa vijana, pia amesisitiza kuwa mtandao wa vitabu uhakikishe vitabu hivi vinafika hadi kwenye shule za vijijini na amehamisisha juu ya ujenzi wa Maktaba na kusaidia kuboresha watoto wetu.
Baadhi ya vijana walioshiriki uzinduzi wa Kampeni ya tusome Tanzania (Let us read Tanzania) wakifuatilia kwa makini hotuba toka kwa mgeni rasmi Mhe. Benjamini William Mkapa (hayupo pichani) leo katika viwanja vya Makao Makuu ya Maktaba ya Mkoa jijini Dar es Salaam.

Let’s read Tanzania Campaign ni kampeni iliyoandaliwa na vijana kutoka hasasi mbalimbali lenye lengo la kuwahamasisha vijana wa kitanzania kujijengea utamaduni wa kupenda kusoma vitabu kwa ajili ya kuongeza fikra za vijana na kuwasaidia katika maisha yao.
Source:Na Benedict Liwenga-Maelezo, Dar es Salaam

Jumatatu, 30 Septemba 2013

MBUNGE WA VITI MAALUM MKOA WA MBEYA. DR. MARY MWANJELWA(CCM), AWACHANGIA LAKI TANO MASHABIKI WA TAWI LA MWANJELWA ENEO LA KABWE




 Juu na chini, Dr. Mary Mwanjelwa akipandisha bendera katika tawi hilo la Mwanjelwa ambako mashabiki wa timu ya Mbeya City, walimwalika kuwa mgeni rasmi.

 Viongozi wa Jiji la Mbeya wakishangilia ilipokuwa ikipanda bendera....
 Mkurugenzi wa Jiji la Mbeya, Mussa Zungiza, akizungumza katika hafla hiyo fupi ya uzinduzi wa tawi la wakereketwa wa timu ya Mbeya City.
 Kulia ni Mwenyekiti wa mashabiki wa Mbeya City FC, Willy Mastala, akifurahia baada ya kukabidhiwa fedha taslmi Tsh. 500,000 na Mbunge wa viti maalum mkoa wa Mbeya, Dr. Mary Mwanjelwa.



 Mbeya City hoyeeeeee..hoyeeeeee...hoyeeeee
 Mashabiki wa tawi la Mbeya City wakiwa pamoja katika hafla hiyo...
 Meya wa Jiji la Mbeya, Athanas Kapunga, akielea protocal za kiuongozi, jambo ambalo vijana walionekana kutomwelewa huku wakipiga kelele za kutofurahia, baadae wakamshangilia baada ya kusema kuwa Jiji litawasafirisha mashabiki kuelekea Arusha tmu hiyo itakapoenda kucheza huko...
 Mbunge Dr. Mary Mwanjelwa akiwa ndani ya uzi wa MBEYA CITY




picha zote kwa hisani ya kalulunga.

Jumamosi, 28 Septemba 2013

RAIS KIKWETE AHUTUBIA MKUTANO UMOJA WA MATAIFA NEW YORK

Rais Kikwete ahutubia Umoja wa Mataifa New York, akutana na Ban Ki Moon, asaini kitabu cha maombolezo ubalozi wa kenya

 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia kikao cha 68 cha Baraza kuu la Umoja wa Mataifa leo jijini New York Marekani.
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia kikao cha 68 cha Baraza kuu la Umoja wa Mataifa leo jijini New York Marekani.
To read his full statement CLICK HERE
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikutana na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban- Ki- Moon ofisini kwake muda mfupi kabla ya kuhutubia kikao cha 68 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa jijini New York Marekani leo mchana. Picha na Freddy Maro
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisaini kitabu cha maombolezo kwenye ofisi za ubalozi wa Kenya wa kudumu katika Umoja wa Mataifa jijini New York jana kufuatia shambulizi la kigaidi katika sehemu ya biashara ya West Gate jijini Nairobi Kenya hivi karibuni.Kulia ni Naibu Balozi wa Kenya wa kudumu Umoja wa Mataifa(Deputy Permanent Representative) Mhe.Koki Muli Grignon.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwafariji wafanyakzi wa Ubalozi wa kudumu wa Kenya katika Umoja wa Kimataifa muda mfupi baada kusaini kitabu cha maombolezo katika ofisi za ubalozi huo jijini New York, Marekani leo mchana kufuatia shambulizi la kigaidi jijini Nairobi ambapo watu kadhaa walipoteza maisha. Picha na Freddy Maro

Alhamisi, 26 Septemba 2013

KANISA LA HOSSANA LIFE MINISTRY UBUNGO RIVER SIDE WATANGAZA SIKU TANO ZA KUFUNGULIWA KWAKILA KILICHOFUNGWA

Mch. kiongozi wa huduma ya Hossana ministry iliyo chini ya Mch. E.R.Mwansasu imetangaza siku tano zakufunguliwa kwakila kilicho fungwa, Mch. Mwansasu ametangaza maombi anayo yaongoza leo ikiwa siku ya pili tangu yaanze wengi wamepokea majibu yao na wanazidi kupokea majibu yao, huduma hii ya Hossana imefanyika faraja kwa wengi kwani imekuwa kituo cha shangwe iliyo hai na kila aliye kimbilia mahali hapa amekuwa akiponywa au kupata jibu lake wakati wasifa na kuabudu.

Mch. Mwansasu anakukaribisha siku yaleo mpaka jumapili kuungana na maelfu ya watu katika maombi yanayo endelea hemani mwabwana.




     Mch. Mwansasu akiimba moja ya ibada kanasani hapo.



TUTAWAENDEA KWA JINA LA BWANA TUTAWASHINDA MAADUI ZETU KISHA TUTARUDI NA MATEKA.


VIJANA WA MKOA WA MBEYA WAMUOMBA MHE. LOWASSA KUWA MGOMBEA URAIS AWAMU IJAYO

Katika jambo ambalo wengi hawakutalajia nipale vijana wa mkoa wa mbeya kupitia mtandao wa kijamii siku ya jana waliandika maneno yanayo onyesha nia ya kumuhitaji Mhe. Lowassa asimame kama mgombea urais awamu ijayo. Vijana hao kupitia Mbeya group wameandika kuwa kama tungekuwa na uwezo tunge mfuata na kumweleza kwamba sisi kama vijana tunamuhitaji awe kiongozi wetu, pia tunge shukuru maana tuna uhakika na yeye katika kile tunacho amini ni tofauti na watu wanavyo mchukulia. Pia wakaongeza kuwa hata katika harakati za kuinuka kiuchumi huyu angetusaidia.



Wengi wanatamani kuwa awe mgombea katika awamu ijayo hasa vijana ndivyo walivyo malizia nakala yao