TAASISI YA VOTER'S VOICE ORGANIZATION (SAUTI YA MPIGA KURA) YAZINDULIWA RASMI DAR ES SALAAM LEO
Steven Mwasomola Mkurugenzi Mkuu wa Voter's Voice Organization.
Mwenyekiti wa Voter's Voice Organization
Alfred Luvanda. (Imeandaliwa na mtandao wa
habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)
Ofisa Mawasiliano wa Voter's Voice Organization,
Andrew Mwakalebela.
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Sauti ya
Mpiga Kura ((Voters Voice Organization), Steven Mwasomola (kushoto),
akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo,
wakati wa hafla ya kuzindua taasisi hiyo. Kulia ni Mwenyekiti wa Jukwaa
la Katiba Tanzania (Jukata), Deus Kibamba.
Mwenyekiti wa Voter's Voice Organization, Alfred Luvanda (katikati), akizungumza katika hafla hiyo ya uzinduzi wa taasisi hiyo. Kulia ni Katibu wa Voter's Voice Organization, Ikupa Njela na Mjumbe kutoka Jukwaa la Katiba Tanzania (Jukata), Hebron Mwakagenda.
Mwenyekiti wa
Jukwaa la Katiba Tanzania (Jukata), Deus Kibamba (kulia), akizungumza
katika uzinduzi huo. Kushoto ni Katibu Mtendaji wa Taasisi ya TAYOAF,
Gasper Mahekuka na Mkurugenzi Mkuu wa Voter's Voice Organization, Steven Mwasomola.
Katibu Mtendaji wa Taasisi ya TAYOAF, Gasper Mahekuka akizungumza katika uzinduzi huo.
Maofisa wa Voter's Voice Organization wakiwa
kwenye uzinduzi huo.
Maofisa wa Voter's Voice Organization wakiwa
kwenye uzinduzi huo.
Dotto Mwaibale
VIJANA nchini wametakiwa kujitokeza
kuhamasisha jamii katika utoaji wa elimu ya uraia na upigaji kura badala
ya kuwaachia wazee wapige kura.
Mwito huo umetolewa na Mwenyekiti wa
Taasisi ya Sauti ya Mpiga Kura (Voters Voice Organization), Alfred
Luvanda wakati akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo,
kwenye hafla ya uzinduzi wa taasisi hiyo.
"Ni vema vijana wakajua elimu ya uraia
na upigaji kura ili kutoa fursa kwa wananxchi wengi kupiga kura katika
chaguzi mbalimbali badala ya kuwaachia wazee"alisema Luvanda.
Alisema watu wengi wanashindwa
kujitokeza kupiga kura kwa sababu hawana elimu ya uraia na upigaji kura
matokea yake wanaochaguliwa kuongoza wanakuwa na idadi ndogo ya watu
waliowachagua.
Akizungumza kuhusu taasisi hiyo, Meneja
Mawasiliano wa Taasisi hiyo Andrew Mwakalebela alisema haifungamani na
chama chochote cha siasa, kidini na mtu yeyote anayeshiriki siasa.
Alisema taasisi hiyo imejikita katika
mambo makuu matatu ambayo ni ya kijamii, Kisiasa na kiuchumi na kutoa
elimu ya uraia na kupiga kura.
Mwakalebela alisema kazi nyingine ya
taasisi hiyo kuimarisha demokrasia ya ukweli kwa kuwaasa wananchi
kuepuka kuuza kura na kuwa chombo cha kuwasemea wananchi pamoja na
kuitangaza amani ya nchi na kuilinda wakati wote.