Ijumaa, 21 Juni 2013

SHETANI ANATAKA KUKUSAIDIA

Pastor Tim Challies. Picha kwahisani ya covenantoflove.net
Makala ifuatayo inatoka kwenye kitabu cha Thomas Books, kiitawacho Precious Remedies Against Satan’s Devices. Kwenye kitabu hicho, ameelezea namna ambavyo shetani anatumia mbinu mbalimbali kukukamata. Gospel Kitaa imetafsiri kitabu hicho kama ambavyo Mchungaji TimChallies wa kanisa la Grace Fellowship lililopo Toronto, Ontario, Canada, alivyoandika kupitia Christian Post.
Anakupa Chambo Huku Akificha Ndoano;
Mara zote, shetani anakushawishi uingie dhambini kwa kukufanya uamini kwamba kile utakachofanya ni kizuri na kina faida, huku akificha upande wa pili wa jambo hilo – upande ambao una madhara, mathalan alipowadanganya Adam na Hawa, hadi wakala tunda. Akili zinafunguliwa kuamini kwamba kuna raha na faida, na pia macho ya mwili hufunguliwa na kupata aibu na kuchanganyikiwa. Yeye aliwaahidi raha na faida, lakini alikuwa na malengo ya pili.
Anapamba Dhambi Kwa Rangi Nzuri
Shetani anajua ya kwamba kama angelikuletea dhambi kama ilivyo, basi kwa hakika ungelikimbia haraka sana bila hata kuitamani. Hivyo anaifungasha dhambi  hiyo ionekane kama ni kitu cha kupendeza chenye maadili ili basi upate kutekwa kwa wepesi, na kuitekeleza kwa raha zako. Anapofanya hivi, majivuno huja kwa namna ionekanayo kuwa ni stahiki, tama ya kumiliki ionekane kama matumizi bora ya pesa, na ulevi kuonekana kama unaenjoy maisha ama vijana wa sasa wanasema ‘unakula good time’. Jaribu lolote ambalo unakutana nalo, atalipamba lionekane si kosa machoni pako.
Anakushawishi kwamba ni dhambi ndogo tu, kitu ambacho kinakusumbua, anakufanya uamini kuwa ni jambo dogo tu na halina madhara. Anakufanya uamini kuwa dhambi hiyo unaweza kuitenda bila kuathiri nafsi yako.
Atakufanya uamini kuwa hata watu wenye heshima zao walitenda dhambi kwa kuficha huzuni na toba yao mbali nawe. Atakufanya uamini kuwa hata watu wakuu wametenda dhambi na bado Mungu anawapenda, atakupa mifano ya uzinzi wa Daudi, majivuno ya Hezekia, Ulevi wa Nuhu, kutovumilia kwa Ayubu, na kuongea hovyo kwa Petro. Lakini anapofanya hivyo, ataficha vilio vyao na kunungunika, na namna ambavyo walitubu kwa dhambi zao na kukutaka usijaribiwe kama wao.
Atakuaminisha kuwa Mungu ana huruma sana

Shetani atakushawishi kutohofu kuhusiana na dhambi anayokuletea mbele yako, na kukuaminisha kuwa hakuna hatari yoyote katika dhambi hiyo, kwa kuwa Mungu ni mwingi wa rehema, na kwamba anafarijika kukusamehe dhambi zako, hachoki kusamehe na kwamba yuko tayari kusamehe muda wowote kuliko kukuadhibu. Anaifunika hukumu ya Mungu
Atakufanya uamini kuwa toba ni rahisi
Shetani anapokuletea jaribu mbele yako, atakuaminisha kuwa kazi ya kutubu ni rahisi, na kwamba sio ngumu kubadilika, kuomba msamaha, kuwa na huzuni na kuomba msamaha wa Mungu, na kama hayo ni kweli, basi hutoona haja ya kupambana na dhambi, kwa kuwa unaweza kutubu baadae kwa urahisi kama ambavyo ulifanya hilo kosa.

Kwa nukuu hizo, unaweza kujitafakari ni mara ngapi umekuwa ukianguka katika dhambi mara baada ya kuwaza mambo yaliyotajwa hapo juu, na huwa unajisikiaje ukishamaliza tukio lako, kitu gani huwa kinakujia akili ni mwako, ni raha ambayo shetani alimuahidi Hawa kule bustanini, ama ni aibu na kujilaumu kama ambavyo ilitokea kwao mara baada ya kula walichozuiwa, anza sasa kujirekebisha, na kila wazo la kutenda maivu linapokujia, basi fikiria madhara yake baadae badala ya kupigwa upofu na kuona kuwa kuna mazuri ndani ya dhambi.

Tukutane wiki ijayo.

Asante GK..

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni