Alhamisi, 26 Septemba 2013

VIJANA WA MKOA WA MBEYA WAMUOMBA MHE. LOWASSA KUWA MGOMBEA URAIS AWAMU IJAYO

Katika jambo ambalo wengi hawakutalajia nipale vijana wa mkoa wa mbeya kupitia mtandao wa kijamii siku ya jana waliandika maneno yanayo onyesha nia ya kumuhitaji Mhe. Lowassa asimame kama mgombea urais awamu ijayo. Vijana hao kupitia Mbeya group wameandika kuwa kama tungekuwa na uwezo tunge mfuata na kumweleza kwamba sisi kama vijana tunamuhitaji awe kiongozi wetu, pia tunge shukuru maana tuna uhakika na yeye katika kile tunacho amini ni tofauti na watu wanavyo mchukulia. Pia wakaongeza kuwa hata katika harakati za kuinuka kiuchumi huyu angetusaidia.



Wengi wanatamani kuwa awe mgombea katika awamu ijayo hasa vijana ndivyo walivyo malizia nakala yao



Hakuna maoni:

Chapisha Maoni